1
Yesu kwa imani, nakutumaini, peke yako, Nisikie sasa, na kunitakasa, ni wako kabisa Tangu leo.
2
Nipe nguvu pia, za kusaidia, moyo wangu, Ulikufa wewe, wokovu nipewe, nakupenda wewe, Bwana wangu.
3
Hapa nazunguka, katika mashaka, na matata, Palipo na giza, utaniongoza, hivi nitaweza kufuata.