13

Umetuahidi

1

Umetuahidi, kwamba wawili, watatu kwa jina lako wakija, Utawabariki, kwa hivi leo twapiga magoti nyumbani pako.

Kiitikio

Yesu uje kwetu, utubariki; Yesu uje kwetu, uwe karibu.

2

Umekuwa nasi, siku nyingine, tunakuhitaji mpaka mwisho, Uje Mkombozi, tupe neema, tusikie Yesu, utubariki.

3

Uje utawale sauti zetu, nyimbo nazo sala, uziagize. Imani izidi, ikamilike, pendo liwe safi na njia nuru.