42

Ewe Roho wa Mbinguni

1

Ewe Roho wa mbinguni, maombi sikia! Makao yako yafanye, mioyoni mwetu.

2

Kama nuru tupenyeze, giza uondoe, Siri yako tuione, na amani yako.

3

Kama moto tusafishe, choma dhambi yetu, Roho zetu ziwe zote, hekalu la Bwana.

4

Kama umande na uje, utuburudishe, Moyo mkavu utakuwa, ni wenye baraka.

5

Kama upepo Ee Roho, katika pentekoste Ukombozi utangaze, kwa kila taifa.