1

U Mtakatifu

1

U Mtakatifu! Mungu Mwenyezi! Alfajiri sifa zako tutaimba, U Mtakatifu, Bwana wa huruma, Mungu wa vyote, hata milele.

2

U Mtakatifu! Na malaika, Wengi sana wanakuabudu wote. Elfu na maelfu, wanakusujudu, Wa zamani na hata milele.

3

U Mtakatifu! Ingawa giza, Lakuficha fahari tusiione, U Mtakatifu! Wewe peke yako, Kamili kwa uwezo na pendo.