2

Twamsifu Mungu

1

Twamsifu Mungu, Mwana wa upendo, Aliyetufia na kupaa juu.

Kiitikio

Aleluya! usifiwe, Aleluya! Amin; Aleluya! usifiwe, utubariki.

2

Twamsifu Mungu, Roho Mtukufu, Akatufunulia Mwokozi wetu.

3

Twamsifu Mwana, aliyetufia, Ametukomboa na kutuongoza.

4

Twamsifu Mungu, wa neema yote, Aliyetwaa dhambi akazifuta.

5

Tuamshe tena, tujaze na pendo, Moyoni uwashe moto wa Roho.