10

Kristo wa Neema Yote

1

Kristo wa neema yote, imbisha moyo wangu, Mifulizo ya baraka, inaamsha shangwe kuu, Unifunze nikupende, nikuandame kote, Moyo wangu ukajae, furaha na tumai.

2

Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku. Salama aniongoza, hata kule nyumbani, Yesu alinitafuta, njiani mbali kwake, Akatoa damu yake, nipone hatarini.

3

Kweli mimi mwiwa mkubwa, wa neema daima Wema wako unifunge, zaidi kwako Bwana, Ili nisivutwe tena, kukuacha ee Mponya, Nitwalie moyo wangu, uwe wako kamili.