100

Kuwatafuta

1

Kuwatafuta wasioweza, kuomba wamrejee Yesu, Kuwaambia maneno yake “Njooni kwangu nawapenda.”

Kiitikio

Nitakwenda (Nitakwenda) niwatafute wapotevu (wapotevu) wageuke, waingie (Waingie) katika zizi la Mwokozi (la Mwokozi)Yesu Kristo.

2

Kuwatafuta wasioweza, waonyeshwe Mwokozi wetu, Kuwaongoza wapate wote, uzima ule wa milele.

3

Kazi hiyo nataka kufanya, leo nimesikia mwito, Kuwainua waangukao, waletwe kwake Yesu njia.