99

Twende kwa Yesu

1

Twende kwa Yesu mimi nawe, njia atuonya tuijue, Imo chuoni na mwenyewe, hapa asema njoo,

Kiitikio

Na furaha tutaiona, mioyo ikitakata sana, Kwako Mwokozi kuonana, na milele kukaa.

2

“Wana na waje,” atwambia, furahini kwa kusikia, Ndiye Mwokozi wetu hasa, na tumtii njoni.

3

Wangojeani? Leo yupo, sikiza sana asemapo, Huruma zake zitwitapo, ewe kijana njoo.