1
Mlangoni pa moyo, mgeni! (amesimama) Amesimama pale, mgeni! (amesimama) Umkaribishe sasa, umkaribishe mwana, Wa Baba wa upendo, mgeni!(umkaribishe)
2
Moyo wako kwa Bwana, fungua. (fungulieni) Asikuache mbali, fungua. (fungulieni) Umkubali Rafiki, roho atafariji, Naye atakutunza, fungua. (fungulieni)
3
Usikie sauti, ya Bwana. (uisikie) Uyachague mambo, ya Bwana. (mambo ya Bwana) Ufungue mlango, usimwambie bado: Jina lake tumai, yu Bwana. (jina la Bwana)
4
Na ufungue moyo, kwa Bwana (fungulieni) Utapewa msaada, wa Bwana (msaada wetu) Uzuri utavikwa dhambi ataondoa, Ukifungua moyo. kwa Bwana (fungulieni)