1
Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami, Moyoni mwetu hungoja hukesha, hukungojea wewe
Kiitikio
“Njoni, kwangu, mliochoka njoni” Yesu huita kwa upole mwingi, akwita, “uje kwangu”.
2
Atuombeapo usikawie, hutuombea sisi, Usidharau wema na huruma, huruma kwetu sisi.
3
Siku za maisha hupita hima, hupita kwako kwangu, Usiku waja kifo kinakuja, huja kwao na kwangu.
4
Fikiri juu ya upendo wake, upendo kwako kwangu; Dhambi zetu amekwisha samehe, msamaha ni wetu.