125

Uniangalie

1

‘Uniangalie’ atwambia, Yesu aliyetufia, Msalabani ni uzima, hapa utaipata hazina.

Kiitikio

Kutazama Kalwari, kutazama Kalwari, Ni kupewa kuishi, kuutazama mti.

2

Ninapojaribiwa ghafula, Shetani hatanitega, Nikitazama msalaba, nguvu nitaipata kwa Bwana.

3

Msalaba nitautazama, kila wakati daima. Ahadi nitategemea, hivi kabisa sitaanguka.