1
Nina haja nawe, kila saa, Hawezi mwingine, kunifaa.
Kiitikio
Yesu nakuhitaji, vivyo kila saa, Niwezeshe Mwokozi, nakujia.
2
Nina haja nawe, kaa nami, Na maonjo haya, hayaumi.
3
Nina haja nawe, kila hali, Maisha ni bure, uli mbali.
4
Nina haja nawe, nifundishe, Na ahadi zako, zifikishe.
5
Nina haja nawe, mweza yote, Ni wako kabisa, siku zote.