151

Huniongoza Mwokozi

1

Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi, Niendapo pote napo, ataniongoza papo.

Kiitikio

Kuongoza hunishika, kwa mkono wa hakika, Nitaandamana naye, Kristo aniongozaye.

2

Pengine ni mashakani, nami pengine rahani, Ni radhi ijayo yote, yupo nami siku zote.

3

Mkono akinishika, kamwe sitanung’unika, Atakachoniletea, ni tayari kupokea.

4

Nikiisha kazi chini, sitakimbia mauti, Kushinda ni ya hakika, nikiongozwa na Baba.