150

Hasha Maneno Mabaya

1

Hasha maneno mabaya, yasitoke kinywani Moyo mwema uzuie, ndimi zisichafuke.

Kiitikio

“Nanyi pendeni,” asema Yesu, (mpendane) (mpendane) Kama mwanzo alivyotupenda, “Nanyi pendeni,” asema Yesu, (mpendane) (mpendane) Wana tiini amri hii (amri heri hii).

2

Pendo ni mtakatifu, urafiki mzuri, Visiharibike mara, kwa kunena vibaya.

3

Tusinene kwa hasira, inazaa huzuni, Pendo lako ee Mwokozi, linatosha tushinde.