1
Baba yetu aliye mbinguni, amenifurahisha yakini, Kuniambia mwake chuoni, ya kuwa nami Yesu pendoni.
Kiitikio
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda, Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.
2
Nimuachapo kutanga mbali, yeye yu vivyo hupenda kweli, Hunirejeza kwake moyoni, kweli yu nami Yesu pendoni.
3
Anipenda, nami ninampenda, kwa wokovu alionitenda, Akanifilia Msalabani, kwa kuwa nami Yesu pendoni.