39

Ati Kuna Mvua Njema

1

Kuna mvua ya baraka, Bwana nimesikia, Unawamwagia wote, bure wanaipata.

Kiitikio

Na mimi, Na mimi, Bwana uninyeshee?

2

Sinipite Baba Mwema, dhambini nimezama, Rehema ni za daima, Bwana, unioneshe.

3

Sinipite, Yesu mwema, niwe nawe daima, Natamani kukwandama, Bwana, unichukue.

4

Sinipite, Roho Mwema, Mpaji wa uzima, Nawe shahidi wa wema, Bwana wema unipe.