1
Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari, Muumba pia wa mbingu, jua nyota mwezi, Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo, Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.
2
Kadiri ya nionayo, ya kusifu Mungu: Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu, Hakuna hata unyasi, usiokukuza, Na upepo wavumisha, au kutuliza.
3
Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa, Ni pato nikusifupo, kukwomba ni dawa, Umenizingira nyuma, na mbele baraka, Maarifa ya ajabu, yanishinda mimi.