1
Hakuna rafiki kama Yesu, hakuna, hakuna, Tabibu mwingine wa rohoni, hakuna, hakuna.
Kiitikio
Yesu ajua shida zetu, daima ataongoza, Hakuna rafiki kama Yesu, hakuna, hakuna,
2
Wakati ambapo hapo yeye, hapana, hapana, Wala giza kututenga naye, hapana, hapana.
3
Aliyesahauliwa naye, hakuna, hakuna, Mkosaji asiyempenda, hakuna, hakuna.
4
Kipawa kama Mwokozi wetu, hakuna, hakuna, Ambaye atanyimwa wokovu, hakuna hakuna.