45

Mlimani Pana Mwanga

1

Mlimani pana mwanga, mwanga wa jua zuri, Shambani na baharini, jua tukufu liko, Mwanga ulio mkubwa, umo moyoni mwangu, Kwa kuwa Yesu alipo, hapa pana mwangaza.

Kiitikio

Mwangaza ulio mzuri, mwanga umo moyoni, Akiwapo Bwana Yesu, pana mwanga moyoni.

2

Kama mavazi kikuu, ninavua huzuni, Nguo nzuri za furaha, umenipa za kuvaa, Nakuandama rohoni, hata nyumba ya juu, Iliyopambwa vizuri, katika pendo lako.

3

Ulinikomboa Yesu, maisha yangu mali, Vyote ni vyako Mwokozi, daima nikusifu, Nakuandama rohoni, hata nyumba ya juu, Iliyopambwa vizuri, katika pendo lako.