1
Ninaye rafiki naye, alinipenda mbele, Kwa kamba za pendo lake, nimefungwa milele, Aukaza moyo wangu, uache ugeuzi, Ninakaa ndani yake, Yeye kwangu milele.
2
Ninaye Rafiki ndiye, aliyenifilia, Alimwaga damu yake, kwa watu wote pia, Sina kitu mimi tena, nikiwa navyo tele, Pia vyote ni amana, ndimi wake milele.
3
Ninaye Rafiki naye, uwezo amepewa, Atanilinda mwenyewe, juu ‘tachukuliwa, Nikitazama mbinguni, hupata nguvu tele, Sasa natumika chini, kisha juu milele.
4
Ninaye Rafiki naye, yuna na moyo mwema, Ni Mwalimu Kiongozi, mlinzi wa daima, Ni nani wa kunitenga na mpenzi wa mbele? Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele