1
Yesu Mwokozi, kwa hakika, hunipa furaha na amani, Mrithi wa wokovu wake, natakaswa kwa damu yake.
Kiitikio
Habari hiyo wimbo wangu, daima nitamsifu Yesu. Habari hiyo wimbo wangu, daima nitamsifu Yesu.
2
Nijitoapo nina raha, na kwa imani namwona Bwana, Aniletea malaika, wananilinda niokoke.
3
Hali na mali anatwaa, katika Yesu nabarikiwa, Nikimngoja kwa subira, wema wake unanitosha.