52

Nipe Biblia

1

Nipe Biblia nyota ya furaha,wapate nuru wasafirio, Hakuna la kuzuia amani, kwani Yesu alituokoa.

Kiitikio

Nipe Biblia neno takatifu, nuru yake itaniongoza, Sheria na ahadi na upendo, hata mwisho vitaendelea.

2

Nipe Biblia nihuzunikapo, ikinijaza moyoni dhambi, Nipe neno zuri la Bwana Yesu, nimwone Yesu Mwokozi wangu.

3

Nipe biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani, Nuru ya neno lake Bwana Yesu, itaangaza njia ya kweli.

4

Nipe Biblia taa ya maisha, mfariji tunapofiliwa, Unionyeshe taa ya mbinguni, nione utukufu wa Bwana.