1
Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu, Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.
Kiitikio
Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.
2
Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia, Anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.
3
Nataka tena zaidi, daima kupambanua, Mapenzi yake nifanye, yale yanayompendeza.
4
Nataka nikae naye, kwa mazungumzo matamu, Nizidi kuwaonyesha, wengine wokovu wake.