1
Walio kifoni nenda waponye, Uwatoe walio shimoni, Wanaoanguka uwainue, Habari njema uwajulishe.
Kiitikio
Walio kifoni, waokoeni, Mwokozi yuko huwangojea
2
Wajapokawia anangojea, Awasubiri waje tobani, Mwokozi hawezi kuwadharau, Huwasamehe tangu zamani.
3
Na ndani ya moyo wa mwanadamu, Huwamo shida tena huzuni, Lakini kwa Yesu kuna rehema, Kuwaponya na kuwaokoa.
4
Walio kifoni nenda waponye, Kazi ni yetu zawadi iko, Nguvu kuhubiri Bwana hutoa, Kwa subira tuwavute sasa.