1
Bwana asubuhi kucha, nitakuinua, Sauti yangu kuomba, nipate baraka.
2
Nakuomba roho yako, niongozwe nayo, Nifanye yanipasayo, na mapenzi yako.
3
Wanaokutegemea, u Mlinzi wao, Matumaini wanayo, utayatimiza.
4
Na kwa wingi wa fadhili, nyumbani mwako juu, Nitaingia na wimbo, pale kusujudu.