1
Mapya ni mapenzi hayo,, asubuhi tuonayo, Saa za giza hulindwa, kwa uzima kuamka.
2
Kila siku mapya pia, rehema wema na afya, Wokovu na msamaha, mawazo mema furaha.
3
Tukijitahidi leo, na mwendo utupasao, Mungu atatueleza, yatakayompendeza.
4
Mambo yetu ya dunia, Bwana atayang’aria, Matata atageuza, yawe kwetu ya baraka.
5
Yaliyo madogo haya, Bwana tukimfanyia, Yatosha tutafaidi, huvuta kwake zaidi.
6
Ewe Bwana siku zote, tusaidie kwa yote, Mwendo wetu wote vivyo, uwe kama tuombavyo.