98

Nilikupa Wewe

1

Nilikupa wewe, damu ya moyoni, Ili wokolewe, winuke ufuni.

Kiitikio

Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini? Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?

2

Nilikupa miaka yangu duniani, Upate inuka, kuishi mbinguni.

3

Nimekuletea, huku duniani, Pendo na wokovu, vyatoka mbinguni.

4

Nipe siku zako, udumu mwangani, Na taabu yako, wingie rahani.

Kiitikio

Nafsi nafsi pendo mali, twae Imanweli. Nafsi nafsi pendo mali, twae Imanweli.