1
Yesu aliniita “Njoo, Raha iko kwangu, Kichwa chako ukilaze, kifuani mwangu,” Nilikwenda kwake mara, sana nilichoka, Nikapata kwake raha, na furaha tena.
2
Yesu aliniita “Njoo, kwangu kuna maji, Maji ya Uzima bure, unywe uwe hai.” Nilikwenda kwake mara, na maji nikanywa, Naishi kwake na kiu, kamwe sina tena.
3
Yesu aliniita “Njoo, dunia i giza, Ukiitazama nuru, ‘takung’arizia. Nilikwenda kwake mara, yeye jua langu, Ni kila wakati mwanga, safarini mwangu.