105

Mchungaji mpenzi

1

Mchungaji mpenzi, hukuita uje, Katika zizi lake, panapo salama, Akina wanawake, waume vijana, Yesu aliye kweli, huwaita kwake.

Kiitikio

Huita kwa moyo wa huruma, ‘uliyepotea uje kwangu,’ Hivi kukungoja anadumu, Bwana Yesu mchunga.

2

Akatoa maisha, kwa ajili yetu, Ataka wapotevu, waje kwake sasa, Tusijihatarishe, kwake tu salama, Sikia wito wake, mchungaji wetu.

3

Tusikawie tena, adui shetani, Kama mbwa wa mwitu, atatuharibu, Tunaitwa na Yesu, mkombozi wetu, Tuingie zizini, panapo nafasi.