106

Ukitafuta Mali

1

Ukitafuta mali, huna wasaa kwa Yesu? Kwa matendo ya haki, huna wasaa kwa Yesu? Anasa za dunia, mambo yako ya raha, Haya unatafuta, huna wasaa kwa Yesu?

2

Mambo yanakusonga, kwake huna nafasi? Watekwa na dunia, kwake huna nafasi? Humwoni m-langoni, anapopiga hodi? Daima hukusihi, kwake huna nafasi?

3

Saa ni za thamani, kwake hamnayo kazi, Wala hamfanyi bidii, kwake hamnayo kazi? Hamkufikia kwao, waliomo shimoni, Na waliopotea, kwake hamnayo kazi?

4

Na wazaa majani tu? Huna tunda kwa Yesu? Mikono i mitupu, huna tunda kwa Yesu? Huna chembe kwa ghala, kazi yako kulipa, Wala huna furaha unapomwona Yesu.