107

Sauti ni yake Bwana

1

Sauti ni yake Bwana, “Kwenda nani tayari? Mavuno yanakawia, nani atayavuna? Kwa kudumu anaita, zawadi atatoa, Nani atakayejibu, “Nipo Bwana nitume.”

2

Kama huwezi safari, hata nchi za mbali, Pana watu karibuni, wasiomjua Yesu, Kama huwezi kusema, jinsi ya malaika, Waweza kuutangaza, upendo wa Mwokozi.

3

Ingawa huwezi kuwa, mkesha mlangoni, Ukiwatolea watu, nafasi ya uzima, Kwa sala na kwa sadaka, watoa msaada, Kama Haruni mwaminifu, kuinua mikono.

4

Roho za watu zikifa, Bwana akikuita, Usiseme kwa uvivu, “Hakuna kazi kwangu.” Kwa furaha anza kazi, ile aliyokupa, Ukajibu mara moja, “Nipo Bwana, nitume.”