108

Tumesikia Mbiu

1

Tumesikia mbiu, Yesu huokoa; Utangazeni kote, Yesu huokoa. Tiini amri hiyo, nchini baharini, Enezeni mbiu hii, Yesu huokoa.

2

Imba nawe askari, Yesu huokoa, Kwa nguvu ya kombozi, Yesu huokoa, Imbeni wenye shida, unapoumwa moyo, Mauti imeshindwa, Yesu huokoa.

3

Mawimbini uenee, Yesu huokoa, Wenye dhambi jueni, Yesu huokoa, Visiwa na viimbe, vilindi itikeni, Na nchi shangilia, Yesu huokoa.

4

Upepo utangaze, Yesu huokoa, Mataifa yashangaa, Yesu huokoa, Milimani, bondeni, sauti isikike, Ya wimbo wa washindi, Yesu huokoa.