1
Anisikiaye aliye yote, sana litangaze wajue wote, Duniani kote neno wapate, atakaye na aje!
Kiitikio
Ni “atakaye,” ni “atakaye,” Pwani hata bara, na litangae, Ni Baba mpenzi alinganaye, atakaye na aje.
2
Anijiliaye Yesu asema, asikawe aje hima mapema, Ndimi njia kweli ndimi uzima, atakaye na aje.
3
Atakaye aje, ndiyo ahadi, atakaye hiyo haitarudi, Atakaye lake ni la ahadi, atakaye na aje.