1
Mlango uko wa wema, mlango wazi huo, Yesu ameufungua, na hakuna kufunga.
Kiitikio
Mlango wazi ajabu, uliachwa wazi kwangu. Kwangu, Kwangu? Wazi wazi kwangu.
2
Mlango hukaa wazi, watu waokolewe. Maskini na matajiri, wa mataifa yote.
3
Maadam mlango wazi, rafiki kaza mwendo, Msalaba ukubali, amana ya upendo.
4
Msalaba tutabeba, daima na furaha, ‘Pendo wa Yesu hushinda, tunainama kwake.