111

Tabibu Mkuu

1

Tabibu mkuu huyu, Yesu mwenye huruma, Atuletaye faraja, Yesu Mwokozi wetu.

Kiitikio

Imbeni malaika, sifa za Bwana wetu, Jina la pekee kwetu, ni la Yesu Bwana.

2

Mwana Kondoo msifuni, msifuni Mwokozi; Hatia zote na dhambi, huziondoa Yesu.

3

Hakuna jina jingine, linalofaa sifa, Au kutufurahisha, isipokuwa lake.

4

Naye atakapokuja, na utukufu wake, Tutafurahi milele, kukaa kwake Bwana.