112

Wewe umechoka sana?

1

Wewe umechoka sana? Wataka raha? Kwake Yesu utapata msaada.

2

Alama anazo yeye? Sana makovu, Ya mikono na miguu na mbavu.

3

Naye amevikwa taji, kichwani mwake? Taji kweli alivikwa miiba.

4

Huku nikimfuata, nipate nini? Maonjo nje na ndani - amani.

5

Kwamba namwandama yeye, mwisho ni nini? Kurithi furaha naye - milele.