113

Damu Imebubujika

1

Damu imebubujika, ni ya Imanweli, Wakioga wenye taka, husafiwa kweli.

2

Ilimpa kushukuru, mwivi mautini, Nami nisiye udhuru, yanisafi ndani.

3

Kondoo wa kuuawa, damu ina nguvu, Wako wote kuokoa, kwa utimilivu.

4

Bwana tangu damu yako, kunisafi kale, Nimeimba sifa zako, ‘taimba milele.

5

Bwana, umenikirimu, nisiyestahili Kwa damu yako sehemu, ya mali ya kweli.

6

Nikubali kukwimbia, mbinguni milele. Mungu nitamsifia, jina lako pekee.