114

Yesu Mwokozi

1

Yesu Mwokozi ili nitakaswe, nataka moyo uwe enzi yako, Ukiangushe kilichoinuka, unioshe sasa niwe mweupe.

Kiitikio

Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi.

2

Bwana Yesu sasa unitazame, unifanye niwe dhabihu hai, Najitoa kwako na moyo vyote, unioshe sana niwe mweupe.

3

Bwana kwa hiyo nakuomba sana, nakungojea miguuni pako, Wanaokuja hutupi kamwe, unioshe sasa niwe mweupe.