1
Naendea msalaba, ni mnyonge mpofu, Yapitayo naacha, nipe msalaba tu.
Kiitikio
Nakutumaini tu, ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako, niponye sasa Bwana.
2
Nakulilia sana, nalemewa na dhambi, Pole Yesu asema, “Nitazifuta zote.”
3
Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu, Roho yangu na mwili, viwe vyako milele.
4
Kwa damu yake sasa, amenivuta sana, Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi.