116

Bwana Ninataka Hili

1

Bwana ninataka hili, kwa kuwa nimechafuka, Kwa moto au kwa maji, unisafishe kabisa.

Kiitikio

Unisafishe Mwokozi, ndani na nje kwa moto, Utakavyo ili dhambi, ife kwangu ife kwangu.

2

Kupewa hekima yote, itakuwa tunu kubwa, Lakini moyo safi ni, bora kwangu bora kwangu.

3

Mpaka moyo ni safi, siwezi kuyafahamu, Mambo mazuri ya mbingu, mambo mazuri ya mbingu.