1
Nilipotoka kabisa, sasa narudi, Nikakawia dhambini, Bwana narudi.
Kiitikio
Narudi nyumbani, daima kwako, Kwa upendo nipokee, naja nyumbani.
2
Nikasusurika sana, sasa narudi, Mwenye uchungu natubu, Bwana narudi.
3
Nimechoka maovuni, sasa narudi, Pendo lako lanivuta, Bwana narudi.
4
Ndilo tumaini langu, sasa narudi, Yesu alinifilia, Bwana narudi.
5
Damu yake yanitosha, sasa narudi, Unioshe kenyekenye, Bwana narudi.