119

Yesu Anasema

1

Yesu anasema, “Wewe huna nguvu, Kesha ukaombe, na uje mwanangu.”

Kiitikio

Alilipa bei, nawiwa naye, Dhambi ilitia waa, aliiondoa.

2

Bwana nimeona, uwezo wako tu, Waweza takasa, mioyo michafu.

3

Sina kitu chema, kudai neema, Hivi nitafua, mavazi kwa damu.

4

Ninaposimama, juu ya mawingu, Taji nitaweka, miguuni pa Yesu.