1
Msalaba wa Yesu, nikae karibu, Pale pana chemchemi, ya kuponya dhambi.
Kiitikio
Pale msalaba, msalaba wake, Huo ni sifa yangu, kwa maisha yote.
2
Karibu msalaba, nalitetemeka, Pendo likaniona, likanirehemu.
3
Unikumbushe Yesu, nikuone pale, Niupate upendo, na kuvutwa nao.
4
Karibu msalaba, kwa kutegemea, Kukesha na kungoja, nitakaa pale.