127

Nionapo Amani Kama Shwari

1

Nionapo amani kama shwari, au nionapo shida, Kwa hali zote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.

Kiitikio

Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu.

2

Ingawa Shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani, Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu.

3

Dhambi zangu zote wala si nusu, huwekwa msalabani, Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.

4

Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia, Utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.