1
Namwandama Bwana, kwa alilonena, njia zangu huning’azia Na nikimridhisha, atanidumisha, taamini nitii pia.
Kiitikio
Kuamini, njia pekee ni hii, Ya furaha kwa Yesu, amini ukatii.
2
Giza sina kwangu, wala hata wingu, yeye mara huviondoa, Woga wasiwasi, sononeko basi, huamini nitii pia.
3
Masumbuko yote, sikitiko lote, kwa mapenzi hunilipia, Baa dhara dhiki, vivyo hubariki, taamini nitii pia.
4
Mimi sitajua, raha sawasawa, ila yote Yesu kumtoa, Napata fadhili, na radhi kamili, taamini nitii pia.
5
Nitamfurahia, na kumtumaini, majumbani na njia-njia; Agizo natenda; nikitumwa huenda, huamini, nitii pia.