129

Kumtegemea Mwokozi

1

Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa, Kukubali neno lake, nina raha moyoni.

Kiitikio

Yesu Yesu namwamini, nimemwona thabiti, Yesu Yesu yu thamani, ahadi zake kweli.

2

Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa, Kuamini damu yake, nimeoshwa kamili. 3. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa, Kwake daima napata, uzima na amani. 4. Nafurahi kwa sababu, nimekutegemea, Yesu mpendwa rafiki, uwe nami dawamu.