1
Yesu kwetu ni rafiki, wambiwa haja pia, Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia, Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya, Kama tulimwomba Mungu, dua alisikia.
2
Una dhiki na maonjo? unamashaka pia? Haifai kufa moyo, dua atasikia, Hakuna mwingine mwema, wa kutuhurumia, Atujua tu dhaifu, maombi asikia.
3
Je hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea, Ujapodharauliwa, njaporushwa pia, Watu wakikudharau, wapendao dunia, Hukwambata mikononi, dua atasikia.