131

Namtegemea Mungu

1

Namtegemea Mungu niwapo, humo barani na baharini, Yeye wa mbinguni anilinda, Baba wa mbinguni anilinda.

Kiitikio

Namwamini, Mungu anitunza (anitunza) Milimani (milimani) au baharini (baharini), baharini Moyo wangu (moyo wangu) aulinda (aulinda), Baba wa mbinguni anilinda.

2

La waridi alinawirisha, na huyo tai juu angani, Nami kweli ananilinda, Baba wa mbinguni anilinda.

3

Tunduni mwa simba namwamini, kwenye vita ama gerezani, Motoni na furikoni, Baba wa mbinguni anilinda.

4

Bondeni mwa giza na upweke, mchunga wangu yu anilinda, Kwa upole aniongoza, Baba wa mbinguni anilinda.