132

Bwana ni Mchunga

1

Bwana ni mchunga sitahitaji, Majani mabichi malisho yangu. Ananinywesha maji matulivu, Atanirudisha nikipotea.

2

Nipitapo bondeni mwa mauti, U mlinzi wangu sitaogopa, Fimbo yako yatosha kunilinda, Ukinifariji sina hasara.

3

Kati ya mateso meza waandaa, Na kikombe changu kinafurika, Umenipaka kichwani mafuta, Nitaulizaje zaidi kwako?

4

Wema na fadhili zinifuate, Siku zangu zote hata milele, Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana, Katika ufalme wa pendo lake.