1
Po pote na Yesu nina furaha, anitumako Yesu ndiyo raha, Asipokuwako hapanifai, akiwapo Yesu mimi sitishwi.
Kiitikio
Po pote, po pote, sina mashaka, Po pote na Yesu, naweza kwenda.
2
Akiwapo Yesu si peke yangu, na nijapotupwa akali wangu Ajaponiongoza njia mbaya, niwapo na Yesu ninashukuru,
3
Akiwapo Yesu naweza lala, naweza pumzika hata kiyama, Kisha nitakwenda kwake milele, akiwapo Yesu furaha tele.